Wachungaji katika maeneo ya ndani sana vijijini mara zote wamekuwa na hali ndogo sana ya kupata vitendea kazi vya kujifunzia Biblia. Wengi wao wana hali ndogo sana ya kusoma Biblia, Hawana mafundisho ya jinsi ya kutafasiri maandiko matakatifu kwa usahihi. Kitabu cha miongozo ya kichungaji ni kitabu rahisi kinachowawezesha wachungaji kuanza kuiendea barabara ya kujifunza theologia ya msingi kwa ajili ya maandalio ya mahubiri, tafasiri za Biblia, na kuelewa wazo kuu la ujumbe wa Biblia ambao ni Kristo mwenyewe.
Ni kitendea kazi chenye kurasa 127 kwa ajili ya watu wale wasio na vyanzo mbalimbali vya mafundisho. Kitabu hiki si cha kushangaza, kigumu au ndo hitimisho. Hata hivyo “Cha faa kwa mafundisho, na kwakuwaonya watu makosa yao, na kuwaongoza, na kuwaadibisha katika haki.” (2 Timotheo 3:16) kwa wale wanaokisoma kwa makini na kukitumia kama kiongozi cha wachungaji kwa ajili ya huduma yenye nguvu.
Zaidi ya yote, wachungaji wengi bado hawajawa ni wafanya wanafunzi. Kitabu hiki kinampa changamoto kila msomaji aweze kuwa ni mtu “anayejizalisha”, mtu ambaye anawekeza muda wake na moyo wake kwa watu wetu. Ni maombi yetu kwamba maelefu ya wachungajui vijijini au maeneo mengine ya mbali duniani wataona kitabu hiki kuwa ni Baraka.
Itakulazimu kuwa na Adobe Acrobat ili uweze kukifungua. Tunapendekeza kwamba utumie Acrobat Reader 7.0 ili uweze kusoma kitabu kizima. Kama huna Adobe Acrobat Reader, basi utaweza kukipata kwa kubonyeza hapa.
Tumegawa kitabu hiki kwa sehemu ndogo ndogo kwa sababu ya ukubwa wake. Hii itarahisisha kufungua sehemu ya kitabu hiki ili uweze kuichapisha au kuisoma tu. Unaweza kufanya hivyo kwa kuchagua sehemu unayohitaji kutoka kwa orodha hii:
Mwongozo Wa Kichungagi – Chuo Cha Biblia Kwa Viongozi (1061K)
Mwongozo Wa Kichungagi
- Jarada
- Yaliyomo
- Utaratibu wa Maandiko
- Mtazamo wa Biblia
- Injiili Ni Nini
- Hadithi Ya Ingiili Na Ufalme Wa Mungu
- Mamlaka ya Maandiko Matakatifu
- Theologia Ya Agano Jipya
- Ni kwa jinsi Gani Agano Jipya linanukuu na kutafasiri Agano la kale
- Utatu
- Jinsi ya Kusoma
- Ubatizo Wa Maji
- Usalama wa Muumini
- Mila Na Injili
- Baraka Na Laana
- Utii wa Imani
- NI KWA JINSI GANI WAWEZA KUTAMBUA
- Theologia ya Somo La Mateso
- Shauku Ya Kitume
- Mahubiri Na John Stott
- Kuandaa Hubiri kutoka katika Neno la Mungu
- TUMEZALIWA ILI TUZAE
- Mchungaji kama mfanya Wanafunzi
- Ufalme Wa Mungu Na Upandaji Makanisa
- Mambo makuu kuhusu Viongozi Wema
- KIONGOZI MTUMISHI
- Utangulizi Wa huduma Ya Ushirika wa Kifalme